Pakua programu ya Starlink (iOS, Android) ili kuangalia ukatikaji, vizuizi, arifa, na taarifa za ziada.

Ruta ya Gen 3
Mwanga wa Ruta wa WiFi:
- Mwanga upo upande wa mbele wa ruta
- Nyeupe Kabisa = Imeunganishwa kwenye intaneti. Utazimika baada ya saa 1
- Mwanga Mweupe Unaomwekamweka = Inajaribu kuunganisha. Mwanga utakuwa mweupe kabisa usanidi utakapokamilika na ruta kuunganishwa kwenye intaneti, au utakuwa mwekundu kabisa ikiwa ruta imeshindwa kupata muunganisho kwenye intaneti kwa dakika 20
- Mwanga wa Urujuani = Ruta iko katika modi ya mchepuko. Utazimika baada ya saa 1. Unahitajika kurejesha mipangilio ya kiwandani ili kutoka kwenye modi ya mchepuko
- Mwanga Mwekundu = Haijaunganishwa kwenye intaneti
- Hakuna Mwanga = Hakuna umeme kwenye ruta. Ikipata muunganisho mzuri, mwanga huo utazimika baada ya saa 1.
Mwanga wa Kigawi cha Umeme:
- LED upande wa chini kushoto mbele wa ruta
Vipimo:
|
|
|
Ruta ya Gen 2/Ruta ya Wavu
Mwanga wa Ruta ya WiFi:
- Mwanga mweupe uko upande wa chini wa ruta. Katika mazingira fulani ya mwanga, mwanga wa taa unaweza kuonekana kuwa na rangi ya bluu.
- Mchoro ulio mbele ya ruta unaonyesha "duaradufu la mzingo wa uhamishaji" la 'Dunia kwenda Mirihi'. Hakuna taa mbele ya ruta
- Mwanga thabiti = Umeme unasambazwa kwenye ruta
- Hakuna mwanga = Hakuna umeme kwenye ruta. Angalia plagi na uhakikishe imechomekwa kikamilifu
Mwanga wa Kigawi cha Umeme:
- Haihusiki - Kigawi cha umeme kimejengewa ndani ya ruta

Ruta ya Gen 1
Mwanga wa Ruta ya WiFi:
- Mwanga uko upande wa mbele wa ruta
- Nyeupe kabisa = Muunganisho mzuri wa intaneti
- Nyeupe inayomwekamweka = Inatafuta setilaiti. Ikiwa ruta haiwezi kupata muunganisho wa intaneti baada ya dakika 20, mwanga utakuwa mwekundu
- Nyekundu = Starlink haijaunganishwa
- Hakuna mwanga = Hakuna umeme kwenye ruta. Angalia muunganisho wa kebo yako kwenye kigawi cha umeme
Mwanga wa Kigawi cha Umeme:
- Taa mbili nyeupe kabisa = Muunganisho mzuri wa umeme
- Mwanga mmoja mweupe umewaka = Hakikisha kila kitu kimechomekwa vizuri na hakuna uharibifu wa zana na vifaa au kebo
- Hakuna mwanga umewaka = Hakuna umeme kwenye kigawi cha umeme. Angalia waya wa soketi na uhakikishe umechomekwa kwenye plagi kikamilifu