Ikiwa umesahau nenosiri lako, huna Programu ya Starlink au unakumbwa na matatizo yoyote wakati wa kusanidi na huwezi kuunganisha kwenye Starlink, unaweza kurejesha mwenyewe mipangilio ya kiwandani ya ruta yako ya Starlink. Kurejesha mipangilio ya kiwandani kutafuta jina la mtandao wako wa WiFi, nenosiri na mipangilio mingine.
Programu ya Starlink (inapendekezwa):
- Unganisha kwenye mtandao wako wa WiFi ya Starlink na ufungue Programu ya Starlink.
- Bofya Mipangilio > Ruta > Rejesha Mipangilio ya Kiwandani.
- Buruta slaidi ili urejeshe mipangilio ya kiwandani ya ruta yako ya Starlink.
Maelezo Muhimu:
- Ikiwa ruta ya Starlink haijahusishwa na akaunti yako au haijaunganishwa kwenye intaneti, maelekezo ya kurejesha mwenyewe mipangilio ya kiwandani yataonyeshwa.
- Kipengele cha kurejesha mipangilio ya kiwandani kwa kutumia Programu ya Starlink hakipatikani ikiwa ruta yako iko katika modi ya mchepuko.
- Jina chaguomsingi la mtandao wa WiFi linaonekana kama 'STARLINK' katika mipangilio ya WiFi ya kifaa.
- Kwa maelezo zaidi kuhusu jina la mtandao wa WiFi na manenosiri, tembelea mada yetu ya usaidizi hapa.
Kurejesha Mipangilio ya Kiwandani kulingana na Ruta:
Ruta Mini:
- Tafuta ikoni na kitufe cha kurejesha mipangilio nyuma ya ruta yako.
- Shinikiza kwa ufupi kitufe ukitumia kitu kama klipu ya karatasi. Mwanga ulio mbele ya ruta unapaswa kumweka haraka kwa sekunde chache.
- Subiri dakika chache ili ruta iwashe upya. LED itamweka polepole rangi nyeupe baada ya ruta kumaliza kuwasha upya.
Ruta ya Gen 3:
- Tafuta ikoni na kitufe cha kurejesha mipangilio chini ya kifuniko cha tundu la LAN nyuma ya ruta yako.
- Shinikiza kwa ufupi kitufe ukitumia kitu kama klipu ya karatasi. Mwanga ulio mbele ya ruta unapaswa kumweka haraka kwa sekunde chache.
- Unganisha kwenye STARLINK kutoka kwenye orodha ya miunganisho ya WiFi inayopatikana kwenye kifaa chako.
- Mara baada ya kuunganishwa, unaweza kusanidi jina na nenosiri la mtandao wako wa WiFi katika mipangilio yako ya programu ya Starlink.
- Fungua programu ya Starlink > Mipangilio > Ruta > weka jina na nenosiri la mtandao wa WiFi unalotaka > Hifadhi.

Starlink Mini:
- Rejesha mipangilio ya kiwandani ya Starlink kwa kubonyeza ikoni ya kuweka upya katika upande wa nyuma.
- Bonyeza kwa uthabiti hadi usikie sauti ya kidoko kisha uishikilie kwa sekunde 3.
- LED itamwekamweka haraka na kuzimika itakapokamilisha.

Ruta ya Gen 2:
- Zima na kuwasha (chomoa plagi kutoka kwenye umeme na kisha uichomeke tena) mara 6 mfululizo takriban muda wa sekunde 2-3 (kwa haraka kama unavyoweza ili kufanikisha kuchomeka na kuchomoa plagi).
- Ruta itachukua dakika chache kuwashwa upya, na itakatiza huduma yako hadi utakapoisanidi tena. Unaweza kutarajia taa iliyo chini ya ruta kuwa nyeupe inayong'aa wakati imekamilika. Hakuna taa mbele ya ruta.
- Unganisha kwenye STARLINK kutoka kwenye orodha ya miunganisho ya WiFi inayopatikana kwenye kifaa chako.
- Mara baada ya kuunganishwa, unaweza kusanidi jina na nenosiri la mtandao wako wa WiFi katika mipangilio yako ya Programu ya Starlink.
- Fungua Programu ya Starlink > Mipangilio > Ruta > weka jina na nenosiri la mtandao wa WiFi unalotaka > Hifadhi.
Ikiwa una nodi zozote za Wavu wa Starlink zilizounganishwa, utahitaji kuzirejesha kwenye mipangilio ya kiwandani baada ya kuweka upya ruta yako kuu.
Wavu - Ruta ya Gen 2:
- Zima na kuwasha wavu (chomoa kutoka kwenye umeme kisha uchomeke tena) mara 6 mfululizo.
- Wakati wa kurekebisha nodi, hakikisha unaunganisha kwenye mtandao wa ruta yako kuu ya Starlink (sio mtandao mpya wa nodi yako ya wavu unaoonekana baada ya kuuchomeka kwenye umeme)
- Fungua Programu ya Starlink. Baada ya dakika 1-2, Programu ya Starlink itakupa kidokezi cha arifa ya "UNGANISHA NODI YA WAVU".
Ruta ya Gen 1:
- Bonyeza kitufe kilicho chini ya ruta kwa upole ukitumia kitu kama klipu ya karatasi.
- Mwanga utageuka kwa muda mfupi kuwa bluu. Subiria taa ya mwanga mweupe kabisa. Ruta itachukua dakika chache kuwashwa upya, na itakatiza huduma yako hadi utakapoisanidi tena.
- Unganisha kwenye STARLINK kutoka kwenye orodha ya miunganisho ya WiFi inayopatikana kwenye kifaa chako.
- Mara baada ya kuunganishwa, unaweza kusanidi jina na nenosiri la mtandao wako wa WiFi katika mipangilio yako ya Programu ya Starlink.
- Fungua Programu ya Starlink > Mipangilio > Ruta > weka jina na nenosiri la mtandao wa WiFi unalotaka > Hifadhi.
Pata taarifa za barua pepe za Starlink hapa.*
Mada Zinazopendekezwa:
Ninawezaje kubadilisha jina la Mtandao wangu wa WiFi (SSID) na nenosiri?