Starlink kwa sasa inatoa mpango wa mwaliko wa wateja nchini Marekani, Australia, Brazili, Chile, Meksiko, Nyuzilandi, Ureno na Uhispania. Wateja wote amilifu wa Makazi na Ughaibuni katika nchi hizi wanastahiki kiotomatiki kushiriki katika mpango wa mwaliko wa wateja.
Kama mtumiaji mpya:
- Ingia kwenye akaunti yako ya Starlink kwenye programu au mtandaoni.
- Katika programu ya Starlink, chagua ikoni ya 'mtu' kisha "Mwezi bila malipo kwako na kwake". (Hii ni "Waalikwa" mtandaoni).
- Unaweza kunakili na kubandika kiungo hiki au kushiriki kupitia programu ya Starlink.
- Rafiki uliyemwalika akinunua kupitia kiungo chako cha mwaliko utapokea arifa kupitia barua pepe.
- Siku 30 baada ya akaunti ya rafiki yako kuamilishwa, muamana wa huduma utatumika kwenye akaunti yako.
- Muamana wa huduma utatumika kupunguza jumla ya ankara yako inayofuata.
Ili kuona ni mara ngapi au kiasi cha muamana wa huduma ambacho kimetumika kwenye akaunti yako, unaweza kuingia kwenye akaunti yako kupitia wavuti na uangalie kwenye sehemu ya mwaliko.

Vizuizi vya sasa:
- Mialiko itatoa tu miamana kwenye usajili wa Makazi na Ughaibuni.
- Misimbo ya mwaliko hutolewa kwenye kiwango cha akaunti, si kulingana na idadi ya laini za huduma.
- Seti zilizonunuliwa kutoka kwa muuzaji rejareja au muuzaji hazistahiki mpango wa mwaliko. Tafadhali kumbuka, hakuna muamana utakaotolewa, hata kama kiungo cha mwaliko kilitumiwa wakati wa uamilishaji.
- Mialiko lazima ifanyike ndani ya nchi moja.
Ninawezaje kutumia muamana wangu wa mwaliko?
- Kama Mwalikwa (Ulijisajili ukitumia kiungo cha mwaliko): Muamana utatumika siku 30 baada ya wewe kuamilisha akaunti yako. Muamana utatumika kiotomatiki kupunguza ankara yako inayofuata. Kwa sababu uamilishaji ni sehemu ya kuhakikisha kwamba mwaliko ni halali, utahitaji kulipia mwezi wa kwanza.