Kuna mipango 2 ya Ughaibuni inayopatikana - Ughaibuni GB50 na Ughaibuni Bila Kikomo.
Ili kuona ikiwa Starlink Ughaibuni inapatikana katika eneo lako:
Maelezo muhimu:
Zana na Vifaa na Waranti: Starlink Performance, Starlink Performance (Gen 2), Starlink Standard na Starlink Mini ndizo Starlink zilizoidhinishwa kwa matumizi ya mwendoni. Wateja wanaotumia Starlink otomatiki ambayo ina mota (kwa mfano, Starlink Standard Otomatiki, Starlink Performance (Gen 1)) wakiwa mwendoni hufanya hivyo kwa hatari yao wenyewe kwani haikuundwa kwa matumizi ya mwendoni; vifaa vinavyoanguka barabarani au nje ya chombo kwa sababu ya kufungwa vibaya vinaweza kusababisha ajali mbaya zinazosababisha jeraha la mwili au uharibifu wa mali. Uharibifu kwa Starlink ikiwa mwendoni unaweza kubatilisha waranti yako ya Starlink. Kwa wateja nchini Japani, zana na vifaa pekee vilivyothibitishwa kwa ajili ya matumizi ya Baharini ni Starlink Performance (Gen 2), Starlink Standard na Starlink Mini. Starlink Standard Otomatiki haijathibitishwa kwa matumizi baharini. Soma Waranti ya Starlink Yenye Masharti kwa maelezo zaidi.
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.