Mipango ya huduma ya Ughaibuni imeundwa kwa matumizi ya mwendoni na ya kuchukulika, kama vile kupiga kambi au kusafiri. Mipango miwili ya huduma inapatikana:
- Ughaibuni GB50, ambayo inajumuisha data ya GB50 na chaguo la kununua data ya ziada kwa GB.
- Ughaibuni Bila Kikomo, ambayo haina kikomo cha data.
** Mipango ya Ughaibuni inajumuisha:**
- Ufikiaji nchini kote, ikiwa ni pamoja na maji ya ndani na bandari, unapatikana katika nchi ya akaunti yako.
- Matumizi ya mwendoni yanaruhusiwa, bila kujali zana na vifaa.
- Mara baada ya kuamilishwa, unaweza kubadilisha mipango ya huduma wakati wowote na mara nyingi kadiri upendavyo kupitia tovuti ya akaunti yako ya Starlink. Mabadiliko yataanza kutumika mara moja au mwanzoni mwa mzunguko wako ujao wa bili, kulingana na mpango.
- Una uwezo wa kusitisha na kuanzisha tena huduma ukitumia Hali ya Akiba (pata maelezo zaidi hapa).
- Usafiri wa kimataifa unaruhusiwa katika masoko yanayopatikana kwa hadi miezi 2 kwa kila safari. Ikiwa unapanga kukaa muda mrefu, unaweza kuombwa uhamishe akaunti yako kwenda nchi mpya. Pata maelezo zaidi hapa.
Maelezo muhimu:
- Watumiaji wa Ughaibuni Bila Kikomo wanaweza kujiandikisha na kulipia Hali ya Baharini* ili kuwezesha ufikiaji zaidi ya maili 12 za baharini au kuunganisha katika maji ya nchi kwa zaidi ya siku 5 mfululizo/kikomo cha siku 60 kwa mwaka mahali ambapo Starlink hutoa ufikiaji amilifu ulimwenguni. Hali ya Baharini pia hutoa kipaumbele cha juu cha mtandao kuliko data ya Ughaibuni kila mahali ambapo Starlink inapatikana.
- Kwa mpango wa Ughaibuni GB50, kumbuka kwamba GB50 ni takriban sawa na saa 20 za utiririshaji wa video ya ubora wa juu au saa 50 za simu za video.
- Ukipitisha data uliyopewa kwenye mpango wa Ughaibuni GB50 na hujajiandikisha kupata data ya ziada, hutaweza kutumia intaneti isipokuwa kufikia akaunti yako ya Starlink, ambapo unaweza kuongeza data ya ziada au kubadilisha mipango.
- Ughaibuni GB50 inapatikana tu katika masoko fulani. Ikiwa Ughaibuni GB50 haitolewi katika nchi yako, tafadhali wasiliana nasi.
- Kwa wateja nchini Indonesia, Malesia, Japani, Jordani na Meksiko, matumizi ya mwendoni ya Starlink kwenye ardhi ni marufuku kwa sababu ya kanuni za eneo husika.
- Ikiwa unatumia Ughaibuni katika nchi tofauti na anwani yako ya usafirishaji kwa zaidi ya miezi miwili, Starlink inaweza kukuhitaji uhamishe akaunti yako kwenda kwenye nchi yako mpya. Ikiwa eneo lako jipya haliko katika eneo lililoidhinishwa (lililo na alama ya "Inapatikana" au "Orodha ya wanaosubiri" kwenye Starlink ramani, huduma yako inaweza kusimamishwa mara moja. Angalia Masharti ya Huduma kwa maelezo zaidi.
- Mpango wa Ughaibuni wa GB10 hautolewi tena. Kwa visa kama hivyo vya matumizi, fikiria GB50 za Ughaibuni kwa data ya kasi ya juu (yenye data ya ziada inayopatikana inayotozwa-kwa-GB) au kusitisha ukitumia Hali ya Akiba kwa data ya kasi ya chini isiyo na kikomo (inayofaa kwa uunganishaji mbadala, ujumbe wa dharura na uamilishaji rahisi hata katika maeneo yasiyo na mawimbi).
- Ikiwa tayari unatumia Ughaibuni GB10, unaweza kuendelea kuitumia. Ikiwa mabadiliko yoyote yatatokea, tutakuarifu mapema ili kufanya mabadiliko yawe rahisi iwezekanavyo. Tafadhali kumbuka kwamba ukibadilisha kwenda kwenye mpango mwingine, hutaweza kurudi kwenye mpango wa Ughaibuni wa GB 10.
*Hali ya Baharini hapo awali ilirejelewa kama Data ya Kipaumbele cha Kimataifa.
Angalia eneo lako kwa ajili ya Starlink Ughaibuni: Agiza Sasa
Pata taarifa za barua pepe za Starlink hapa.
Mada Zinazopendekezwa:
Ninawezaje kubadilisha mpango wangu wa huduma?
Je, ninaweza kutumia Starlink "mwendoni"?
Kwa nini sipati mpango wangu wa huduma?